Enzo Maresca amesisitiza kuwa anataka Raheem Sterling abaki Chelsea lakini akakiri The Blues watalazimika kuwauza wachezaji ili kupunguza kikosi chao kilichojaa.
Mkufunzi mpya wa Chelsea Maresca alisisitiza kutojumuishwa kwa Sterling kwenye kikosi kitakachomenyana na Manchester City ilikuwa ni “uamuzi wa kiufundi”, licha ya kukerwa kwa mshambuliaji huyo wa Uingereza.
“Kitu pekee ninachoweza kusema tena ni uamuzi wa kiufundi, sio zaidi ya hilo,” alisema Maresca.
“Namtaka Raheem Sterling, lakini nataka wachezaji wote 30 tulio nao, lakini hakuna nafasi kwa wote. Kwa hivyo, kwa baadhi yao, lazima waondoke.
Axel Disasi, Ben Chilwell na Carney Chukwuemeka wote hawakuwapo kwenye kikosi cha mechi ya Chelsea, na hivyo kumuacha Maresca akiwa na wachezaji zaidi wa kusimamia utawala huo.