Wadukuzi mjini Tehran walifanikiwa kupokea barua pepe za ndani kutoka kwa timu ya mgombea wa chama cha Republican. Kampeni ya Biden-Harris pia ililengwa.
“Iran inataka kuzusha mifarakano na kudhoofisha imani katika taasisi zetu za kidemokrasia.
Siku yaJumatatu, Marekani ilihusisha rasmi udukuzi uliolenga kampeni ya Donald Trump dhidi ya Tehran. Ile ya Joe Biden na Kamala Harris pia ililengwa – kabla ya Biden kujiondoa – bila mafanikio.
“Tumeona vitendo vya uchokozi vinavyozidi kufanywa na Iran wakati wa mzunguko huu wa uchaguzi”, unaolenga haswa “kuhatarisha kampeni ya rais wa zamani Trump, na ambayo idara za ujasusi inaihusisha Iran”, imebainishwa katika taarifa ya pamoja kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Ujasusi wa taifa (ODNI), Polisi wa Shirikisho (FBI) na shirika la Usalama wa Mtandao na Miundombinu (CISA).
Kampeni ya Donald Trump, ambayo ilifichua shambulio la Agosti 10, ilikuwa imeishutumu Iran.
Kulingana na ripoti ya Microsoft, kundi la wadukuzi la Mint Sandstorm, ambalo linafanya kazi chini ya uongozi wa idara za kijasusi za Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, lilifanikiwa kutumia shambulio la hadaa.
Afisa wa kampeni ya Donald Trump alibofya kiungo katika barua pepe iliyotumwa kutoka kwa akaunti iliyoathiriwa ya mshauri wa zamani.
Hii iliwezesha wadukuzi kuelekeza upya shughulii kwenye kikoa kilicho chini ya udhibiti wao, na kupata hati nyingi za ndani.
Vyombo kadhaa vya habari vya Marekani, vikiwemo Politico na Washington Post, vilipokea ripoti ya kurasa 271 kuhusu udhaifu unaowezekana wa mgombea mwenza wa Donald Trump, J.D. Vance, na sehemu ya memo kuhusu Marco Rubio – ambaye alikuwa kwenye orodha fupi ya kuandamana na Trump.