Belarus ilisema Jumatatu ilituma ndege, vikosi vya ulinzi wa anga na ghala la silaha kwenye mpaka wake na Ukraine, siku moja baada ya Rais Alexander Lukashenko kusema kuwa ametuma karibu theluthi moja ya vikosi vya jeshi la nchi yake katika eneo hilo.
“Kundi limeongezeka kwa kiasi kikubwa, na kwa sasa wako kazini katika mipaka ya kusini mwa nchi yetu,” Kamanda wa Jeshi la Anga na Ulinzi wa Anga wa Belarus Meja Jenerali Andrei Lukyanovich, aliambia shirika la utangazaji la CTV linalomilikiwa na serikali.
Tangazo hilo linakuja muda mfupi baada ya dikteta wa Belarus Alexander Lukashenko kusema kuwa ametuma theluthi moja ya jeshi la taifa hilo mpakani msimu huu wa joto.
Lukasjenko alidai kuwa kuongezeka kwa wanajeshi kwenye mpaka ni matokeo ya kutoelewana kati ya Belarusi na Ukraine.
Kyiv haijathibitisha madai ya Lukyanovich kuhusu askari wa ziada wa Belarusi na silaha kwenye mpaka.