Marioo ametangaza kusitisha kampeni za kuutangaza wimbo wake mpya “iPhone Users” kutokana na baraza la sanaa taifa (BASATA) kumtaarifu kuwa wimbo huo hauajazingatia maadili.
Marioo amesema “ni kweli Basata wameniambia wimbo wangu wa “iphone users haujazingatia Maadili na nilipokea taarifa hiyo siku tatu Baada ya wimbo kutoka, hivyo mpaka leo suala lipo barazani.
Hivyo ndio maana sijaendelea na promotion wala kitu chochote kuhusu project hiyo” ameandika kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram, Insta-Story.
Siku 13 zimepita tangu wimbo huo utoke rasmi, ukiwa na watizamaji zaidi ya laki tatu You Tube (393k) na unashika nafasi ya nane katika Trendings kwenye mtandao huo.
iPhone Users ni moja kati ya nyimbo itakayokua katika albamu mpya ya msanii huyo inayotarajiwa kuachiwa hivi karibuni, tunaendelea kuwatafuta BASATA kufahamu wimbo huo umekiuka maadili yapi.