Haki ya kupata Taarifa au Uhuru wa kupata Habari inaelezwa kuwa ni Haki ya Mtu yeyote kuuliza Taasisi ya Umma ili kupata Taarifa zinazohusu Huduma za Umma, Matumizi ya Fedha za Umma n.k.
Uhuru wa kupata Taarifa unahusisha vipengele viwili Vikuu ambavyo ni wajibu wa kutoa Taarifa, na Haki ya kupata Taarifa.
Hivyo, Wananchi wana Haki ya kuomba na kupokea Taarifa, na Serikali ina wajibu wa kuchapisha/kutoa Taarifa hizo mara kwa mara Haki hii kwa sehemu fulani inaweza isipatikane, tena kwa Nyaraka ambazo zinalinda Usalama wa Taifa kukiwa na tafsiri inayoeleweka kuhusu Usalama wa Taifa
Wananchi wanapopata Taarifa (Access To Information) kuhusu Serikali yao inavyofanya kazi, wanaweza kuitumia Haki yao ya Uhuru wa Kujieleza kwa manufaa zaidi.
Haki ya kupata Taarifa ni sehemu muhimu ya Demokrasia na inahusiana kwa karibu na Haki nyingine muhimu za Binadamu ikiwemo Uhuru wa Kujieleza.
Serikali zinapaswa kufanya Kazi kwa maslahi bora ya Wananchi.
Wananchi wanapopata Taarifa kuhusu shughuli za umma, huweza kufanya tathmini ikiwa Viongozi wanatimiza ahadi zao na kufanya Maamuzi wakiwa na Taarifa sahihi.
Nchi mbalimbali zina wajibu wa kuweka mazingira wezeshi kwa wananchi kutafuta, kupokea na kusambaza taarifa na mawazo, jukumu linalohusisha pia kutunga sheria zitakazosimamia haki ya kupata taarifa, kulinda wafichua uhalifu, kushughulikia kashfa kwa kutumia sheria za madai badala ya za jinai, na zisizotoa fidia kubwa kupita uhalisia katika maisha ya kawaida.
Katika kudhibiti maudhui ya mtandaoni, nchi zina wajibu wa kuzuia baadhi tu ya maudhui hayo, kama vile picha au maelezo yanayohusu ngono zinazohusisha watoto wadogo, na kauli zinazochochea chuki, ugaidi au mauaji ya halaiki.