Mwanamume mmoja anashikiliwa na polisi kama sehemu ya uchunguzi uliofunguliwa baada ya kugunduliwa kwa mafuvu 17 ya vichwa vya binadamu mwishoni mwa mwezi wa Julai, katika eneo linaloshukiwa kuwa patakatifu katikati mwa Uganda, polisi imetangaza hivi punde siku ya Jumanne Agosti 20, 2024.
Mtu huyu “alitafutwa kuhusiana na mafuvu ya vichwa vya binadamu ambayo yalipatikana hivi majuzi kwenye moja ya nyumba yake huko Mpigi”. “Alikamatwa Jumatatu na yuko kizuizini,” msemaji wa polisi Kituuma Rusoke ameliambia shirika la habari la AFP.
Watoto waliokuwa wakitafuta kuni nje ya kijiji cha Kabanga katika wilaya ya Mpigi, takriban kilomita 40 magharibi mwa mji mkuu wa Kampala, waligundua ugunduzi huo mbaya Julai 28, wakaazi walisema. Mafuvu hayo yalipatikana katika chumba cha chini ya ardhi kilichoko kwenye kilima.
“Kikosi cha polisi cha upelelezi wa uhalifu kilipata taarifa na wakamkamata Lujja Bbosa Tabula mnamo Agosti 19,” msemaji wa polisi Kituuma Rusoke aliambia AFP Jumanne, akisema yupo kizuizini.
“Tabula alikuwa akitafutwa kuhusiana na mafuvu ya vichwa vya binadamu viliyokutwa katika makazi yake huko Mpigi hivi karibuni,” alisema.
Rusoke alisema Tabula atafikishwa mahakamani mara upelelezi utakapokamilika. Hajaweka wazi tarehe ya kufikishwa mahakamani.
Bado haijulikani jinsi mafuvu ya kichwa yaliishia sehemu hio, iliyoko kwenye juu ya mlima, na iliyozikwa ndani ya masanduku manne ya chuma ndani ya chumba kilicho chini ya ardhi kwa undani wa mita mbili (futi saba).