Zaidi ya maambukizi 1,000 mapya ya Mpox, ambayo kwa muda mrefu yaliitwa monkeypox, yamerekodiwa katika muda wa wiki moja nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kulingana na ripoti kutoka kituo cha kudhibiti magonjwa cha Umoja wa Afrika, Africa CDC, iliyotolewa siku ya Jumanne.
Shirika la afya la Umoja wa Afrika (AU) pia lina wasiwasi kuhusu kusambaa kwa virusi hivyo katika nchi jirani za Burundi na Jamhuri ya Afrika ya Kati
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) inasalia kuwa nchi iliyoathiriwa zaidi na janga hilo na takriban kesi 18,000 zimerekodiwa tangu kuanza kwa mwaka 2024, ikijumuisha zaidi ya kesi mpya 1,000 katika wiki iliyopita. Nchi imeunda mpango wa dola milioni 49 kwa ajili ya kukabiliana na mlipuko huo, fedha za kwanza ambazo zilitangazwa jioni ya Jumanne Agosti 20 kufuatia mkutano wa dharura. Inatosha kuwahakikishia mamlaka juu ya udhibiti wa haraka wa virusi hivi.
Waziri wa Fedha wa DRC Doudou Fwamba ametangaza dola milioni 6 za kwanza za mpango wa dola milioni 49 na “anatumai kuwa washirika kadhaa” watajiunga na mpango huo.
Lakini Daktari Jean Kaseya, mkurugenzi mkuu wa Afrika CDC, pia anabainisha kuenea kwa wasiwasi katika mataifa kadhaa jirani.
“Tahadhari inakuja kutoka Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambapo tunaona ongezeko la idadi ya vifo na kesi mpya. Hata kama hakuna nchi mpya zilizoathiriwa, virusi hivyo vinaendelea, sio tu barani Afrika, bali pia katika mabara mengine.