Kutokea Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam leo imeanza kusikilizwa rufaa ya Juma Magoma dhidi ya Klabu ya Yanga kuhusu kupinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambayo iliipa ushindi klabu hiyo.
Itakumbukwa mbali na madai mbalimbali ya Magoma na mwenzake Geofrey Mwaipopo na Abeid Mohamed Abeid mahakama iliwaamuru wamlipe muombaji ( Bodi ya Wadhamini ya Klabu ya Yanga) gharama za uendeshaji wa shauri hilo.
Hata hivyo, rufaa hiyo ambayo ipo mbele ya Jaji Salma Maghimbi imeahirishwa hadi Agosti 30, 2024 ambapo nje ya mahakama tumeongea na Wakili wa Magoma, Jacob Mashene
“Kesi imeitishwa kwa ajili ya kutajwa na amri ya mara ya mwisho ilitutaka sisi tupeleke wito kwa Fatmah Karume na Jacob Katunzi ambapo tuliwapelekea wito na leo mawakili wao wamefika mahakamani lakini mawakili wa Yanga wamekuja na mapingamizi wakitaka mahakama iyasikilize kabla ya rufaa ya msingi sisi tukawa tayari kwa ajili ya tarehe nyingine na si ya leo,”.