Mwenyekiti wa ANGE (Tume ya kitaifa ya Kusimamia Uchaguzi) Ahmed Barticheret ametoa tangazo hilo lilitolewa Jumatano Agosti 21, 2024 .
Fomu za kugombea katika chaguzi hizo zitawasilishwa kuanzia Oktoba 19 hadi 28, 2024 na matokeo ya mwisho yatajulikana Februari 3, 2025. Kalenda hii inachapishwa siku tano baada ya kutangazwa kwa sheria inayoanzisha muundo wa Bunge.
Kwa mujibu wa Mahamat Zen Bada, katibu mkuu wa MPS, chama tawala, wanaharakati wako tayari: “Mwishoni mwa mazungumzo, tuliambiwa kuwa mpito ulikuwa wa miaka miwili. Kwa hiyo miaka miwili nni mwisho wa 2024. Lazima kabisa turudi kwenye utaratibu wa kikatiba. ”
Kulingana na Mchungaji Moyadé Narédoum, rais wa chama cha ADIL, mazingira ya sasa ya kisiasa na kiuchumi ya nchi hayatoa nafasi nzuri kwa upinzani. “Ni mwendo wa kasi. Na ninaamini kwamba hii haitusaidii kuelekea kwenye amani nchini Chad. ”
Kwa mashirika ya kiraia, kalenda hii haikubaliki. Jean Bosco Manga, mmoja wa watu mashuhuri wa mashirika ya kiraia nchini Chad anasema: “Tunalazimishwa kufanya uchaguzi, kwa sababu hatuwezi kuandaa uchaguzi bora bila kusuluhisha maswali ya mgawanyiko [wa uchaguzi] ambayo yamekosolewa hadi sasa” .
Wakati huo huo, chama cha Succès Masra Transfoma kinajiandaa kwa kongamano mwezi Septemba mwaka huu ili kutayarisha makataa haya ya uchaguzi.
Muungano wa mashirika ya kiraia dhidi ya dhuluma na ukosefu wa usawa na Kundi la Ushauri la wadau wa Kisiasa (GCAP) wanaongoza kampeni ya kukataa sheria hii inayoanzisha muundo wa Bunge.