Jeshi la Urusi siku ya Alhamisi lilidai kuwa lilikuwa limeteka kijiji kingine katika eneo la mashariki mwa Ukraine la Donetsk, ikiwa ni eneo la hivi punde zaidi katika msururu wa maeneo kwa wanajeshi wa Moscow.
Wizara ya ulinzi mjini Moscow ilisema kuwa vikosi vyake viliteka kijiji cha Mezhove, kilichoko kati ya Avdiivka, kilichotekwa mwezi Februari, na kitovu cha vifaa cha Pokrovsk, ambako wanajeshi wa Urusi wanasonga mbele.
Urusi pia ilisema siku ya Alhamisi ilizuia mashambulizi kadhaa ya ndege zisizo na rubani na makombora ya Ukraine magharibi mwa nchi hiyo, likiwemo eneo la Volgograd ambapo moto ulizuka katika kituo cha kijeshi, kulingana na mamlaka za eneo hilo.
Ulinzi wa anga “ulizima shambulio la ndege isiyo na rubani kwenye eneo la mkoa wa Volgograd katika eneo la Marinovka, ndege nyingi zisizo na rubani ziliharibiwa,” gavana wa eneo hilo Andrei Botcharov alisema kwenye Telegraph.
Kufuatia ajali ya kifaa kimoja kati ya hivi, “moto ulizuka katika eneo la kituo cha Wizara ya Ulinzi” kabla ya kuzimwa, Botcharov aliongeza, akionyesha kwamba hakukuwa na majeruhi.