Msanii wa kizazi kipya Omary Ally Mwanga Maarufu kama Marioo mapema leo ameitikia wito na kufika katika ofisi za Baraza la Sanaa la Taifa lengo ikiwa ni kufanya majadiliano na Katibu Mtendaji wa @basata.tanzania Dkt. Kedmon Mapana kuhusiana na sakata la wimbo wake wa “Iphone users” alioutoa Msanii huyo kuwa na maneno yaliyoleta utata katika jamii
Mara baada ya kufika alipokelewa na Katibu Mtendaji na kufanya kikao cha majadiliano kati ya viongozi wa BASATA na uongozi pia wa Msanii huyo
Katika kikao Katibu Mtendaji wa BASATA Dkt. Mapana ametumia fursa hiyo kuwataka Wasanii wazingatie na kuusoma Mwongozo wa maadili katika kazi za Sanaa ambao ulitolewa na BASATA, huku akieleza kuwa mwongozo huo unapatikana katika tovuti ya BASATA, Aidha Katibu Mtendaji pia alimkabidhi Mwongozo huo Msanii @marioo_tz huku akimtaka akafanye marekebisho katika nyimbo yake ya Iphone user.
Pia Katibu Mtendaji amewataka Wasanii nchini kuwa kioo cha Jamii kwa kufanya kazi zao kwa kuangalia mila na desturi huku wakiwa mabalozi wazuri katika kueneza na kudumisha utamaduni wa nchi yetu ya Tanzania.
Kikao hicho kimefanyika leo Agosti 22, 2024 katika ofisi za BASATA zilizopo Jengo la Utumishi Jijini Dar es salaam.