Mamlaka za forodha na ulinzi wa mipaka nchini Marekani zimenasa dawa za kulevya aina ya “methamphetamine” yenye thamani ya dola milioni 5 (Tsh. bilioni 13,498,090,820) ambayo ilikua imefichwa katika shehena kubwa ya matikiti maji.
CBP ilimuhoji dereva wa lori aliyekua amebeba shehena hiyo mwenye umri wa miaka 29 ambaye alikuwa akivuka kuelekea Marekani kutoka Mexico Ijumaa ya wiki iliyopita, baada ya mahojiano ya awali waligundua biashara ya matunda ya mtu huyo inahitaji uchunguzi zaidi.
Uchunguzi wa karibu mpaka sasa umebaini kuwa “tikiti maji” alizokua amebeba mwanaume huyo zilikuwa na vifurushi 1,220 vya “methamphetamine” vilivyofungwa kwa karatasi ya kijani iliyochapishwa ambayo ni nadra mtu kuigundua.
Usafirishaji wa jumla ulikuwa na uzani wa paundi 4,587 (kilo 2,080), na thamani inayokadiriwa ya zaidi ya $ 5 milioni (Tsh. bilioni 13,498,090,820).