Mwanamke wa Kijapani mwenye umri wa miaka 116, Tomiko Itooka sasa ndiye mtu mzee zaidi duniani, Guinness World Records ilitangaza Jumatano, Agosti 21, 2024.
Itooka anatwaa rekodi hiyo baada ya mwanamke mwingine aliyekua akiishikilia kutoka Uhispania, Maria Barnyas Morera kufariki wiki hii akiwa na umri wa miaka 117.
Itooka, aliyezaliwa Mei 23, 1908, alikuwa akiishi katika kituo cha kuwatunza wazee huko Ashiya, jiji la Hyōgo, mkoa wa Japani, kwa miaka mitano, kabla ya kurudi nyumbani kwa binti zake wawili.
Kulingana na Guinness World Records, Itooka alilelewa pamoja na kaka zake huko Osaka, ambapo alisoma shule ya msingi na upili. Kufikia umri wa miaka 20, aliolewa na mume wake, na wenzi hao walikuwa na watoto wanne pamoja.
Mwanamke huyo anapendelea kula ndizi, kinywaji cha maziwa kila asubuhi, alikua mchezaji wa voliboli akiwa sekondari, amezaa mabinti wawili na watoto wa kiume wawili, na aliwahi kukaa mwenyewe kwa kipindi cha miaka 10.