Mahakama ya wilaya ya wilaya ya mbulu mkoani manyara imeshindwa kutoa hukumu dhidi ya mchungaji wa mifugo carol christopher(18) mkazi wa kijiji cha moringe kata ya daudi anaekabiliwa na shtaka moja la kumlawiti mtoto mwenye umri wa miaka miwili na miezi tisa baada ya kushindwa kufika kusikiliza hukumu yake iliyopangwa kutolewa agosti 21 mwaka huu.
Upande wa mashtaka safari hii ukiongozwa na mwendesha mashtaka mkaguzi wa polisi maraba masheku badala ya mwendesha mashtaka katika shauri hilo kiongozi mkaguzi wa polisi wakili hamilton mosses aliiomba mahakama hiyo kuwa upo tayari kwa mshtakiwa kusikiliza matokeo ya shauri lake linalomkabili.
Lakini mama wa mshtakiwa carol bi anna burra aliyekuwa amemshikia kijana wake dhamana aliiomba mahakama hiyo kuwa mshtakiwa ameshindwa kufika kusikiliza hukumu dhidi yake baada ya kusumbuliwa ugonjwa wa tumbo la kuhara na hivyo amelazwa katika hospitali ya seriani mkoani arusha hvyo atahakikisha anamleta mahakamani hapo agosti 26 kwa amri ya mahakama.
Ingawa mdhamini bi burra hakuonyesha kielelezo chochote aidha pia kutoulizwa kuonyesha kielelezo cha vyeti vinavyothibitisha kuugua kwa mashtakiwa carol mbele ya meza ya hukumu ya hakimu,mkazi mwandamizi mfawidhi mh johari kijuwile wa mahakama hiyo mdhamini huyo alisisitiza kuwa alilazwa tangu agosti 19 mwaka huu.
Kwa upande mwingine hakimu kijuwile alipotaka kufahamu atapewa ruksa lini ili mahakama hiyo iweze kutoa maamuzi? mdhamini burra ameiambia mahakama hiyo kuwa kwa kuwa hali ya mshtakiwa sio mbaya ataweza kufika baada ya siku tatu.
Hata hivyo hakimu kijowile amemuamuru mdhamini bi anna bura kutii amri ya mahakama anahakikisha anamfikisha mshakiwa carol christopher agosti 26 majira ya saa 3:00 asubuhi akiwa na vielelezo vya hospitali ya selian vinavyothibitisha mshtakiwa alikuwa amelazwa na kupatiwa matibabu kwenye hospitai hiyo.
Shauri hilo limefikia tamati baada ya upande wa utetezi katika mahakama hiyo kufunga utetezi uliowasilisha mashahidi watatu ambao pia walionekana kuwa waongo huku upande wa mashtaka kuwasilisha mashahidi sita’
Awali mwendesha mwendesha mashtaka katika shauri hilo kiongozi mkaguzi wa polisi wakili hamilton mosses mashtaka akisoma hati ya mashtaka alisema mshtakiwa carol christopher(18) amesema mnamo juni 13 majira ya saa tisa alasiri katika kitongoji cha getagu alimwingilia isivyo halali na bila ya ridhaa yake mtoto mwenye umri wa miaka miwili na miezi tisa na kisha kumlawiti katika eneo la malisho alikokuwa akichunga ng’ombe na hivyo kukamatwa.