Uwepo wa ongezeko la mmonyoko wa maadili vitendo vya ukatili pamoja na unyanyasaji kwa watoto umetajwa kusababishwa na baadhi ya wazazi kushindwa Kuishi na watoto badala yake kuwaachia wasichana wa kazi jali ambayo imesababisha watoto wengi kukosa Malezi yaliyo bora.
Wito huo umetolewa na diwani kata ya Mji Mpya Mhe. Emmy Kila katika kuhitimisha mashindano ya mtoto bomba amesema kuwa ipo haja ya kuandaa makongamano mbalimbali yatakayoweza kuwakutanisha watoto na kuwapa elimu juu ya ukatili unaofanywa na kusababisha kuharibika kwa watoto.
Amesema siku za hivi karibuni kumekuwa na matukio mengi ya ukatili Kwa watoto ikiwemo kubakwa ,kulawitiwa na kuuawa hivyo wazazi lazima wawe mstari wa Mbele kukemea matukio haya.
Kwa Upande wake Paschal Elias mkurugenzi wa mashindano ya mtoto bomba amesema kuwa kwa kutambua jitihada zinazofanywa na Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania chini ya Dkt Samia Suluhu Hasani wameunga Mkono na kuanzisha mashindano haya yenye lengo la kuinua vipaji pamoja na kutoa elimu kwa watoto dhidi ya ukatili.
Hata hivyo ameziomba Serikali pamoja na wadau mbalimbali kushirikiana katika mashindano haya ikiwa lengo kuu ni kupunguza na kumaliza ukatili kwa watoto pamoja na kuandaa na kutengeneza kizazi kilicho Bora.
Naye Koplo wa polisi (CPL) Suleiman Ibrahim Kova wa Dawati la Jinsia amewataka wazazi kukaa na watoto wao na kuacha kuwategemea walimu wao kwa asilimia kubwa kwani mtoto ana nafasi kubwa ya kumweleza mzazi wake juu ya mambo mabaya anayofanyiwa.
Mashindano ya mtoto bomba yalianza tangu julai 1 na kutamatika agost 24 huku shule mbalimbali kutoka Mkoani Morogoro zikishiriki na yanatarajia kufanyika tena Disemba 2024 yakiambatana na matukio mbalimbali kama kwenda kutoa msaada katika vituo vya watoto yatima mkoani Morogoro.