Barcelona wameanza msimu wa LaLiga vyema kwa kushinda mara mbili mfululizo licha ya kuwakosa wachezaji kadhaa muhimu, jambo linaloongeza matarajio ya meneja mpya Hansi Flick.
Kuwapo kilelen LaLiga pamoja na Celta Vigo kwa pointi sita, Barcelona watasafiri hadi Madrid kumenyana na Rayo Vallecano Jumanne, ambao hawajafungwa baada ya kuwashtua Real Sociedad 2-1 na kuwabakisha Getafe sare tasa siku ya Jumamosi.
“Lengo la Barcelona linapaswa kuwa kushinda ligi kila wakati,” Flick aliambia mkutano na waandishi wa habari Jumatatu.
“Ni kweli ni safari ndefu, lakini tumeanza vizuri japo kila kitu kinaweza kubadilika haraka, sasa tunafuraha kwa kuanza kwetu na tunajiamini, hatutazamii Mei mbele, lengo letu ni kuweka kasi katika mchezo ujao. .
“Tumeridhika sana na kile ambacho timu inafanya uwanjani. Ubora wa vipindi vya mazoezi ni mzuri, wachezaji wana umakini mkubwa, nguvu ni nzuri … na unaweza kuona katika mechi.”