Wananchi zaidi ya mia mbili katika kijiji cha Losinon Kata ya Oljoro namba 5 Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara wamefanya maandamano nakufunga barabara kwa zaidi ya saa sita wakiishinikiza serikali kutatua changamoto ya ukosefu qa maji ambayo wameipata kwa zaidi ya miaka 30
“Tunataka Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa afike aone tunavyoumia,kuna mama mmoja alijifungua pale zahanati akavuja damu sana lakini ikaitwa Ambulance impeleke hakuna maji,maji tunayotumia ni maji taka”-Naini Mkazi wa kata ya Oljoro namba 5
Meneja wa Ruwasa wilayani Simanjiro Mkoani Manyara Johanes Martin ametoa ahadi ya miezi miwili kutatua changamoto hiyo ikiwa ni pamoja na kulaza mabomba na kuanz kuwasambazia maji