Rais wa zamani Donald Trump ametishia kujiondoa katika mdahalo uliopangwa na mgombea mpinzani Kamala Harris kwenye mtandao wa TV wa Marekani ABC, huku pande zote mbili zikitofautiana kuhusu iwapo vipaza sauti vibaki moja kwa moja katika kipindi chote cha tukio.
Timu ya makamu wa rais inashinikiza vipaza sauti vya wagombea wote wawili kuwashwa hata mgombea mwingine anapozungumza, tofauti na wakati wa mdahalo wa CNN mwezi Juni.
Kwa upande mwingine Kamala Harris ameonyesha kupanda katika kura za maoni, akionekana kuwa na nafasi nzuri zaidi ya kushinda dhidi ya Donald Trump.
Harris ameimarisha nafasi zake katika majimbo muhimu kama Arizona, Georgia, na Pennsylvania, huku akielekea kupata kura 241 kati ya 538 zinazohitajika kwa ushindi.
Katika Seneti, Wademocrats wanakabiliwa na changamoto, huku WRepublican wakiwa na asilimia 67 ya kushinda wingi. Hata hivyo, Harris anaendelea kupata uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa Wademocrats.
Wapiga kura wa Trump wanafikiria kwamba huenda Harris akapata ongezeko dogo baada ya kikao cha chama chake na wanasema kuwa inabidi waangalie hali ya kura katika majimbo lengwa ili kufikia lengo la kura 270 zinazohitajika kwa ushindi.