Katibu Mkuu wa Jumuiya ya wazazi CCM Taifa Ally Hapi amepokelewa kwa kishindo mkoa Njombe baada ya kuwasili mkoani humo kwa ziara ya siku nne yenye lengo la kuijenga jumuiya ya wazazi na chama cha Mapinduzi kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wananchi kushiriki katika zoezi la uhuishaji wa Taarifa zao katika Daftari la Mpiga kura pamoja na kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa,vijiji na vitongoji utakaofanyika Novemba 27 mwaka huu.
Hapi akiwa mkoani Njombe atatembelea wilaya za kuoa huo huku akikutana na mabalozi katika ngazi ya shina,wenyeviti wa vijiji na kufanya mikutano ya wananchi ambapo atapokea kero mbalimbali za wananchi ili kuzitafutia majibu katika ngazi zinazohusika
Baada ya Kuwasili mkoani Njombe Hapi amewaomba viongozi wa Chama Chama Mapinduzi CCM kutoa ushirikiano katika siku zote nne atakazokuwepo mkoani humo kwani itachochea ukuaji wa chama na kukifanya kiendelee kuaminiwa na wananchi
“Mimi pamoja na wenzangu tumekuja hapa mkoani njombe,tunashukuru kwa mapokezi yenu makubwa mliyotupa hakika mmetuonesha upendo wa dhati kwetu na kwa chama chetu,tutakuwa hapa kwa takribani siku nne za kutembelea katika maeneo mbalimbali ambako tutafaya kazi za kutembelea mashinda kushuhudia kazi ya chama inavyofanywa lakini pia tutahamasisha wananchi kushiri katika uchaguzi wa serikali za vijiji na vitongoji”alisema Hapi
Mbali na hayo Hapi alisema katika ziara hiyo watapata nafasi ya kueleza kazi zinazofanywa na serikali ya chama cha mapiduzi CCM Chini ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan tangu ameingia madarakani katika kuwaletea maendeleo wananchi ikizingatiwa kuwa serikali imetoa mabilioni ya fedha katika mkoa wa njombe kwaajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo katika kila sekta na kila wilaya.