Lionel Messi atakosa mechi zijazo za Argentina za kufuzu Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Chile na Colombia kutokana na jeraha, huku Paulo Dybala akirudishwa kwenye kikosi cha kocha Lionel Scaloni Jumatatu.
Messi hajaichezea klabu ya Inter Miami tangu alipoumia kifundo cha mguu katika ushindi wa 1-0 wa Argentina dhidi ya Colombia kwenye fainali ya Copa America.
Mshambulizi wa Roma, Dybala hajacheza mechi ya kimataifa tangu Machi 2023 lakini anaweza kupata fursa ya kuongeza mechi 38 kama Messi hayupo.
Mabingwa hao watetezi wa dunia pia watamkosa Angel Di Maria baada ya winga huyo mkongwe kustaafu kimataifa.
Argentina kwa sasa wako vinara wa Amerika Kusini wanaofuzu kwa dimba la 2026 nchini Marekani, Canada na Mexico.