Viongozi wa makanisa Yerusalemu wameeleza wasiwasi waao mkubwa kuhusu vita vya Israel dhidi ya Gaza, wakihimiza pande zinazohusika kufikia makubaliano ya haraka ya kusitisha mapigano.
Taarifa yao inasema kuwa hali katika Palestina imeendelea kuzorota licha ya wito wa kusitisha mapigano. Milioni ya wakimbizi wanakabiliwa na hali mbaya, nyumba zao zimeharibiwa, na mamia ya watu wanakufa au kujeruhiwa kila wiki kutokana na mashambulizi yasiyo na kipimo. Wengine wanakabiliwa na njaa, kiu na magonjwa.
Viongozi hao wa makanisa wamewataja viongozi wa pande zinazohusika kwenye mgogoro huu kuwa na wasiwasi zaidi kuhusu masuala ya kisiasa kuliko kumaliza mchakato wa amani. Huku wakihimiza kufikiwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano kwa haraka, kuachilia mateka, na kurudisha wakimbizi katika nyumba zao.
Mazungumzo ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Hamas yanaendelea Cairo, huku juhudi za upatanishi zikikwama kutokana na wa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kukataa kutekeleza matakwa ya Hamas.
Vita hivyo vimepelekea zaidi ya vifo 40,400 vya Wapalestina na majeruhi zaidi ya 93,500, huku kizuizi cha muda mrefu kikiathiri upatikanaji wa chakula, maji safi na dawa.
Israel inakabiliwa na mashtaka ya mauaji ya kimbari katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki na kizuizi kikiwa kimeathiri zaidi ya Wapalestina milioni moja waliokuwa wamepata hifadhi katika jiji la Rafah kabla ya kuvamiwa.