Hakimu wa mahakama nchini Marekani amemnyima dhamana mshukiwa wa mauaji ya Tupac Shakur mwaka 1996 huko Los Angeles.
Kiongozi wa zamani wa genge la Los Angeles anayeugua hivi sasa, Duane “Keffe D” Davis, ndiye mtu pekee aliyewahi kushtakiwa kuhusiana na ufyatuaji risasi uliogharimu maisha ya nyota huyo wa hip-hop.
Kiongozi huyo wa zamani wa genge hilo ameomba kuachiliwa kwa dhamana, iliyowekwa ya $750,000, mara kadhaa tangu kukamatwa kwake Septemba 2023 na amekabiliwa na kunyimwa mara kwa mara.
Katika kukataa ombi lake la hivi punde, Jaji Carli Kierny alitaja wasiwasi kuhusu uhalali wa fedha zinazotolewa ili aachiliwe.
Alisema alikuwa na mashaka juu ya uwazi wa fedha hizo, na kupendekeza kuwa juhudi zingekuwa zinaendelea kuficha asili yao halisi.
Sheria ya Nevada inakataza wauaji waliopatikana na hatia kunufaika kifedha kutokana na uhalifu wao.
Davis amekana hatia ya mauaji ya daraja la kwanza mpaka hivi sasa.