Klabu ya Al Hilal na Bayern Munich zimeripotiwa kufikia makubaliano ya uhamisho wa winga Mfaransa Kingsley Coman kwenda Saudi Arabia.
Pendekezo la mabingwa hao tayari limepokelewa na Bayern na lilionekana kukubalika kwa wababe hao wa Ujerumani kulingana na Fabrizio Romano.
Walakini, mpango huo bado haujakaribia kukamilika. Coman hakuamua kama anataka kuhamia Saudi Arabia na bado anasubiri vilabu vya Ligi Kuu ya Uingereza. Miamba wa Catalan Barcelona pia walionyesha kumtaka winga huyo wa Ufaransa katika siku chache zilizopita.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 pia alikuwa akitakiwa na Al-Ahli Jeddah mapema katika dirisha la usajili lakini sasa wanaonekana kuwa na nia ya kumsajili mshambuliaji wa Uingereza Ivan Toney.
Al-Hilal bado hawajafanya usajili mkubwa majira ya joto, huku wachezaji wake wote wa kigeni wa msimu uliopita bado wapo klabuni hapo, wakiwemo Renan Lodi, Neymar, Sergej Milinkovic Savic, Aleksandar Mitrovic, Kalidou Koulibaly, Yassine Bounou, na Ruben Neves.