Siku ya Sept 7 mwaka huu itakua ni Jumamosi imetengwa kutoa faraja kwa familia na watu wa karibu wa wasanii wote waliotangulia mbele za haki ambao wameacha alama kwa njia moja au nyingine hapa nchini
Siku hiyo ambayo itakua maalumu kwa familia hizo huku zikisomwa dua na maombi kutoka watumishi wa Mungu tofauti tofauti akiwemo Mwamposa, watakuwepo wasanii Mbali Mbali wa filamu na Muziki, watangazaji na waandishi wa Habari Pamoja na viongozi Mbali Mbali
AyoTVENT imezungumza na mmoja waandaaji wa tukio hilo ambaye ni Steve Nyerere amesema “Tukio hilo linatarajiwa kufanyika katika viwanja vya leaders Kinondoni kuanzia saa 3 Asubuhi, kutakuwa na dua na ibada kutoka viongozi wa Dini, lakini pia kuwashika mkono na kuwapa faraja wafiwa ambao ni Ndugu wa karibu na Jamaa”
#millardayoENT