Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema serikali inaendelea kufanya udhibiti wa vileo vinavyoingia nchini na kuathiri vijana na kupelekea kushindwa kufanya kazi kwa ulevi uliopitiliza.
Waziri mkuu Majaliwa amesema hilo bungeni jijini Dodoma katika kipindi cha maswali kwa waziri wakati akijibu swali la Saashisha Mafuwe, Mbunge wa Jimbo la Hai aliyetaka kujua kauli ya serikali kuhusu kudhibiti uingizwaji wa vileo vikali vinavyoathiri uchumi wa vijana na uchumi wa nchi
“serikali inaendelea kutoa elimu kwa jamii yetu ya kupunguza na kuonyesha madhara ya ulevi uliopitiliza ikiwemo na hiyo aliyosema mbunge Vijana wengi wanalewa wanashindwa kufanyakazi hivyo tunaendelea kutoa elimu ya stadi za maisha kwa vinaja hawa lakini muhimu zaidi ni kutoa elimu ya ujasiliamali kwa vijana hawa kwa lengo la kuwaonyesha vijana hawa njia nzuri na sahihi watakayojishughulisha na kuhakikisha wanapata pato kuliko njia jii ya kuendelea kunywa viroba ambavyo baadae vitamlaza siku nzima hana mtaji na hawezi kupata mafao” PM Majaliwa