Rais wa Rwanda Paul Kagame amewafuta kazi takriban wanajeshi 214 wakiwemo maafisa kadhaa wakuu wa kijeshi.
Taarifa fupi ya Wizara ya Ulinzi ya Rwanda, iliyowekwa kwenye ukurasa wake rasmi wa X asubuhi ya leo, ilisema kuwa maafisa waliofutwa kazi ni pamoja na Meja Jenerali Martin Nzaramba na Kanali Dkt Etienne Uwimana.
“Pia ameidhinisha kufutwa na kubatilishwa kwa maafisa 195 wa vyeo vingine vya Jeshi la Ulinzi la Rwanda,” ilisema taarifa hiyo.
Hakuna sababu iliyotolewa kwa hatua hiyo, lakini ilitangazwa saa chache baada ya Kagame kukutana na maafisa wakuu wa kijeshi, akiwemo Mkuu wa Majeshi Jenerali Mubarakh Muganga.