Mtandao wa kijamii wa X unakabiliwa na kusimamishwa kufanya kazi nchini Brazil baada ya kushindwa kutimiza makataa ya saa 24 ya mahakama.
Siku ya Jumatano, jaji wa Mahakama Kuu ya Brazil alionya kwamba X inaweza kusimamishwa kazi ikiwa Mkurugenzi Mtendaji Elon Musk hatateua mwakilishi mpya wa kisheria kwa shughuli za jukwaa hilo nchini Brazil ndani ya saa 24.
Siku ya Ijumaa, X alitangaza kuwa inatarajia kufungwa nchini Brazil baada ya kukosa tarehe ya mwisho ya kutimiza matwakwa ya mahakama.
“Hivi karibuni, tunatarajia Jaji Alexandre de Moraes ataamuru X kufungwa nchini Brazili – kwa sababu tu hatutatii amri zake zisizo halali za kuwadhibiti wapinzani wake wa kisiasa,” timu ya X ya Global Government Affairs ilisema katika taarifa.
Kampuni hiyo ilisisitiza kuwa haisisitizi nchi nyingine kupitisha sheria za uhuru wa kujieleza sawa na Marekani.
“Suala la msingi lililopo hapa ni kwamba Jaji de Moraes anadai tuvunje sheria za Brazil wenyewe. Hatutafanya hivyo,” taarifa hiyo iliongeza.
X pia alitangaza mipango ya kuchapisha “madai yote yanayodaiwa kuwa haramu ya Jaji de Moraes na kesi zinazohusiana na mahakama kwa maslahi ya uwazi,” akisisitiza kujitolea kwake kupinga kile anachokiona kuwa ni kinyume cha sheria.
“Tofauti na mitandao mingine ya kijamii na majukwaa ya teknolojia, hatutatii kwa siri maagizo yaliyo kinyume cha sheria,” kampuni hiyo ilisema.