Baada ya serikali ya Zanzibar kupitia shirika la Bima Zanzibar kuyataka mashirika ya ndege na abiria kutakiwa kukata Bima ya Lazima kwa Abiria waingiao nchini bima ambayo inatarajiwa kukatwa kwa $44
ni miezi kadha tangu Serikali kuanzisha utaratibu huo ukiwa na lengo la kuwakinga na majanga, utaratibu ambao unatarajiwa kuanza Octoba mosi, ambapo pia Serikali kupitia shirika la Bima Zanzibar imepanga kuhamishia utaratibu huo kwenye vyombo vya Majini vinavyofanya Safari znz ,Dsm na pemba ambapo Mtalii atalazimika kua na Bima hiyo
“Tulianza kukaa na kampuni za Airline pamoja na mamlaka za viwanja vya ndege,lakini leo tumeenda kwenye upande mwingine ambapo wageni wengine watakua wanapitia kama Entry Port wakati wakufika Zanzibar ,tumewapa taarifa kuhusu bima ya usafiri ya lazima ambayo inatarajiwa kuanza Octoba Mosi tumeona kuna umuhimu wa kukaa na wadau wa sekta ya usafirishaji wa majini na kuwapa taarifa —Hamida Juma”