Morocco imezindua sensa ya 7 ya Watu na Makazi (RGPH) kwa lengo la kukusanya data sahihi kuhusu idadi ya watu na hali ya makazi nchini humo.
Sensa hii, inayoongozwa na Tume ya Juu ya Mipango (HCP), inafanyika kwa kiwango cha kitaifa kuanzia Septemba 1 hadi 30.
Lengo la Sensa hii ni kutoa mwangaza wa kina kuhusu idadi ya watu wa Morocco na hali zao za maisha. Inahusisha matumizi ya kompyuta ndogo na maswali ya ufahamu, ili kukusanya data kutoka kwa kila kaya.
Kampeni hii imehusisha rasilimali kubwa za kibinadamu na vifaa, ikiwa ni pamoja na washiriki 55,000, kompyuta ndogo 55,000, na vifaa vya sensa 55,000. Bajeti ya operesheni hii inakadiriwa kuwa Dirhamu bilioni 1.46 za Kimorocco ambazo ni sawa na shilingi Bilioni 390 za Kitanzania.
Sensa hiyo itatoa mwangaza muhimu kuhusu muundo wa demografia, ulinzi wa kijamii, matumizi ya teknolojia ya habari, na hali ya mazingira. Taarifa zitakazokusanywa zitatumika kufuatilia malengo ya maendeleo endelevu na kutoa mwongozo wa maamuzi ya sera.