Vikosi vya Urusi vilianzisha shambulizi lingine kubwa dhidi ya Kyiv, na kurusha makombora zaidi ya 20 katika mji mkuu wa Ukraine usiku wa kuamkia muhula mpya wa shule.
“Vikosi vya ulinzi wa anga viliharibu zaidi ya makombora kumi na mbili na takriban makombora kumi na mbili ya balestiki na ndege isiyo na rubani angani juu ya Kyiv,” Serhiy Popko, mkuu wa utawala wa kijeshi wa mji wa Kyiv, alisema katika taarifa ya asubuhi siku ya Jumatatu.
Kulingana na Popko, shambulio hilo lilisababisha moto mwingi huku vifusi vikianguka katika wilaya nne za Kyiv ambapo Watu wawili walijeruhiwa.
Kyiv haikuwa shabaha pekee ya vikosi vya Rais wa Urusi Vladimir Putin kwa usiku mmoja.
Urusi ilirusha, kwa jumla, makombora 35 ya baharini na ya balestiki na drones 23 katika mikoa ya Kyiv, Kharkiv na Sumy.
Jeshi la anga la Ukraine limeripoti kudungua makombora 22 na ndege zisizo na rubani 20.
Huko Sumy, eneo linalopakana na Kursk ya Urusi ambako Ukraine inaendesha mashambulizi yake ya kuvuka mpaka, vikosi vya Urusi vilishambulia kituo cha ukarabati wa kijamii na kisaikolojia wa mayatima, utawala wa kijeshi wa eneo hilo uliripoti.
Hata hivyo, wakazi 18 wa nyumba za jirani walijeruhiwa, wakiwemo watoto sita, wanawake tisa na wanaume watatu,” ofisi ya mwendesha mashtaka wa eneo hilo ilisema.