Papa Francis aliwasili nchini Indonesia Jumanne kwa ziara ya siku tatu katika nchi hiyo yenye Waislamu wengi zaidi duniani ambapo anatarajiwa kusisitiza uhusiano kati ya dini mbalimbali.
Papa Francis aliwasili Indonesia yenye Waislamu wengi siku ya Jumanne kuanza ziara ya mataifa manne ya Asia-Pasifiki ambayo itakuwa ndefu na ya mbali zaidi ya upapa wa mzee huyo mwenye umri wa miaka 87.
Mkuu wa Wakatoliki bilioni 1.3 duniani aliwasili Jakarta kwa ziara ya siku tatu inayohusu mahusiano ya kidini, na kisha atasafiri kwenda Papua New Guinea, Timor Mashariki na Singapore.
Ziara hiyo ya siku 12 itapima afya ya papa inayozidi kudhoofika, lakini mara nyingi anatiwa nguvu kwa kuwa miongoni mwa kundi lake na katika wiki za hivi karibuni ameonekana mwenye ari nzuri.
Papa alipaswa kuwa na siku ya kustarehe mjini Jakarta Jumanne kufuatia safari ndefu ya ndege kutoka Roma, kisha kukutana na Rais Joko Widodo siku ya Jumatano katika sehemu kuu ya kwanza ya ziara yake katika nchi hiyo yenye Waislamu wengi zaidi duniani.