Jamii nchini imetakiwa kuendelea kuweka misingi imara ya elimu ya fedha kuanzia ngazi ya chini ili kuepusha kuzalisha jamii ambayo itashindwa kuwa na nidhamu ya fedha pamoja na vyanzo sahihi kupata mitaji kwa manufaa yao.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam wakati wa mafunzo ya elimu ya fedha kupitia Taasisi ya Hazina Saccos ambapo mtendaji mkuu wa Taasisi ya Hazina Saccos Festo Mwaipaja amesema ili kunusuru jamii na mikopo riba pamoja na changamoto nyengine katika sekta ya fedha ni lazima kujenga misingi imara kuanzia ngazi ya chini ikiwemo katika shule.
” Bado jamii zetu nyingi zipo nyuma sana sisi kama Hazina Saccos tumeona tuje na hili la kutoa mafunzo kwa kuanzia ngazi za shuleni hadi kufika mitaani kwa lengo la kuwaingezea maarifa juu ya fedha, lakini pia tunahitajika kuinusuru jamii na mikopo riba pamoja na changamoto nyengine katika sekta ya fedha ni lazima kujenga misingi imara kuanzia ngazi ya chini” Amesema Mwaipaja.
Naye Daniel Mwakyambiki ambaye ni katibu mkuu wa saccos ya hazina na mkuu wa shule amezitaja shule zitakazo nufaika na mradi hiyo kwa sasa ni katika halmashauri ya jiji la Dar es Salaam pamoja na Kinondoni lakini wanataraji kufika Tanzania nzima, ambapo moja ya elimu inayifundishwa ni namna ya kuhifadhi na kuweka akiba ya fedha.
Hata hivyo nao baadhi ya wanafunzi ambao ni wanufaika wa mradi huo wamesema itawasaidia kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha pamoja na kujua namna ya kuwekeza katika vyama vya akiba na mikopo pindi watakapoanza kujitegemea.