Chini ya usimamizi wa Elon Musk, katika jukwaa la X [Twitter] umewaacha wawekezaji wake kupata hasara kubwa za kifedha kwa mujibu wa ripoti.
Wakati Elon Musk aliponunua X (wakati huo Twitter) mnamo 2022 kwa dola bilioni 44, alifanya hivyo kwa kuungwa mkono na kundi kubwa la wawekezaji, akiwemo Mwanamfalme wa Saudi Alwaleed bin Talal, mwanzilishi mwenza wa Twitter Jack Dorsey na kampuni zinazoongoza za ubia za Silicon Valley.
Bw Musk na kundi lake la wawekezaji wameripotiwa kupoteza zaidi ya dola bilioni 24 katika thamani ya karatasi kwenye uwekezaji wao, gazeti la Washington Post liliripoti. Thamani ya kampuni imeshuka kwa asilimia 72 tangu Oktoba 2022.
Kulingana na uchanganuzi wa Washington Post, vitega uchumi vinane vikubwa zaidi vya awali vimepoteza kwa pamoja takriban dola bilioni 5 za thamani tangu kuchukuliwa kwa Bw Musk.
Dau la jumla limepoteza thamani ya dola bilioni 24, huku wawekezaji kama Jack Dorsey, Larry Ellison na Sequoia Capital wakikabiliwa na hasara kubwa.