Waziri Mkuu wa DRC Judith Suminwa alitembelea gereza kuu la Makala siku ya Jumatano, Septemba 4, ambapo wafungwa 129 walifariki usiku wa Septemba 1 kuamkia Septemba 2 wakati wafungwa walipokuwa wanajaribu kutoroka na kisha polisi kuingilia kati kwa kutumia nguvu kupita kiasi kulingana vyanzo kadhaa. Mkurugenzi wa gereza amesimamishwa kazi.
Joseph Yusufu Maliki amesimamishwa kazi na Waziri wa Sheria, Constant Mutamba.
Sasa anafanyiwa uchunguzi wa kina na mamlaka ya Kongo na waranti wa kumtafuta umetolewa dhidi yake, huku wafungwa 129 wakipoteza maisha katika gereza la Makala usiku wa Jumapili Septemba 1 kuamkia Jumatatu Septemba 2, kulingana na mamlaka ya Kongo.
Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vilivyohojiwa na RFI, Joseph Yusufu Maliki alitangaza jana, Jumatano Septemba 4, kuwa ni mgonjwa, hivyo kuhalalisha kutokuwepo katika gereza la Makala. Hata hivyo, vyanzo vingine vinadai kuwa tayari ametoroka nchi.