Cristiano Ronaldo alifikia hatua kubwa kwa kuwa mchezaji wa kwanza wa soka kufunga bao lake la 900 katika maisha yake ya soka wakati wa mchezo wa Ureno dhidi ya Croati na hii ilitokea katika mechi ya UEFA Nations League iliyofanyika Lisbon
Cristiano Ronaldo alifunga bao la 900 katika maisha yake ya ajabu siku ya Alhamisi wakati Ureno ilipoichapa Croatia 2-1 mjini Lisbon katika mchezo wao wa kwanza wa UEFA Nations League.
Ronaldo, 39, alifunga krosi ya Nuno Mendes katika dakika ya 34 ya mechi hiyo kwenye Uwanja wa Estadio da Luz na kufikia kilele.
Alionekana mwenye hisia aliposherehekea bao hilo, likiwa ni goli lake la 131 katika jezi ya Ureno.
Nusu ya mabao yake aliifungia Real Madrid, huku mabao yaliyosalia yakienea katika muda wake wote akiwa Sporting Lisbon, Manchester United na klabu ya sasa ya Al-Nassr.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 39 sasa amefunga mabao 131 ya kimataifa, 450 akiwa Real Madrid, 145 akiwa na Manchester United, 101 akiwa na Juventus na 68 kwa klabu yake ya sasa ya Al Nassr na pia matano kwa klabu yake ya kwanza ya Sporting Lisbon.
Mchezaji wa Argentina Lionel Messi, wa pili katika orodha ya wafungaji wa muda wote, amefunga mabao 859 katika maisha yake ya soka.
Bao la Diogo Dalot liliwaweka Ureno mbele mapema kabla ya Ronaldo kufunga, huku bao la kujifunga la Dalot likipunguza idadi ya mabao kabla ya mapumziko.
Timu hizo ziko katika Kundi A1 la toleo la hivi punde zaidi la Ligi ya Mataifa pamoja na Poland na Scotland.
Ureno itaikaribisha Scotland mjini Lisbon siku ya Jumapili.