Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis anatarajiwa kuwasili nchini Papua New Guinea baadaye leo, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ndefu zaidi kuwahi kutokea nje ya nchi.
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis anatarajiwa kuwasili nchini Papua New Guinea baadaye leo, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ndefu zaidi kuwahi kutokea nje ya nchi kwa lengo la kuwafikia Wakatoliki katika pembe za mbali za dunia.
Ziara ya siku tatu ya Papa Francis nchini Papua New Guinea itamfikisha katika mji mkuu wa Port Moresby ambapo atakutana na viongzi wa nchi, jumuiya za kiraia na viongozi wa makanisa. Kiongozi huyo atashiriki katika misa ya Jumapili kabla ya kuelekea mji wa mbali wa Vanimo kukutana na wamisionari wa Kikatoliki.
Papua New Guinea ni nchi kubwa na iliyozungukwa na milima, misitu na mito ikiwa na makabila ya mwisho ya jamii za asili. Vatikani inakadiria kuwa kuna takriban Wakatoliki milioni 2.5 nchini humo.