Uongozi wa Chama cha Soka Wilaya ya Morogoro (MDFA) umevunjwa kwa kukiuka taratibu za uchaguzi wakati wa kuchagua viongozi hao ambapo zoezi la uchaguzi ulifanyika pasipo mabadiliko ya katiba kuidhinishwa na msajili vya wa vyama vya michezo Taifa.
Uongozi wa Chama cha Soka umevunjwa ukiwa umehudumu kwa kipindi cha miezi sita, tayari ukiwa umetekeleza majukum mbalimbali ikiwemo kuratibu mabonanza ya michezo ya kuwaendeleza vijana kisoka, kwasasa kunao uongozi wa mpito viongozi 09 ambao wameteuliwa kuhudumu kwa kipindi cha siku 90 hadi uchaguzi mwingine tena utakapofanyika
wakizungumza na vyombo vya Habari Viongozi waliochaguliwa kusimamia michezo Mkoani Morogoro wameahidi kwenda kusimamia vyema na kuondoa migogoro yote ikiwemo kusimamia kwa haki uchaguzi ujao
Ramadhani Wagala ni mwenyekiti wa mpito katika watu 09 waliochaguliwa kusimamia mpira na amesema kuwa yeye pamoja na wajumbe wake nane waliochaguliwa watasimamia Shughuli za soka kwa muda wote ikiwemo kuratibu uchaguzi utakaopaswa kufanyika ndani ya uongozi wao
Leo hii umefanyika mkutano wa pamoja wa Viongozi hao wa mpito na wajumbe wa vilabu wa vyama vya soka Wilaya ya Morogoro, ikielezwa kuvunjwa kwa uongozi huo ni matokeo ya kutotii katazo la wasimamizi wa michezo wilaya kufanya uchaguzi pasipo katiba kuidhinishwa.
Kinachofaanyika sasa ni uongozi huo unasimamia majukumu yote ya chama na kufanikisha uchaguzi mpya wa viongozi.