Maafisa wa Shirika la Taifa la Kupambana na Dawa za Kulevya (NDLEA) la Nchini Nigeria, wamekamata shehena ya Madawa ya kulevya yaliyofichwa kwenye Pedi za kike na vyombo vya kutunzia mafuta ya nywele yakiwa yanaelekezwa nchini Uingereza, Ireland na Cyprus.
Katika taarifa iliyotolewa Jumapili na msemaji wa shirika hilo, Femi Babafemi, ilielezwa kuwa, katika moja ya Makampuni ya usafirishaji, vifurushi 30 vya Cocaine vyenye uzito wa kilogramu 1.1 vilikamatwa katika vyombo vya kutunzia Mafuta ya nywele, vinavyoelekezwa Ireland mnamo Septemba 3, 2024.
Vifurushi vingine 24 vya Cocaine vyenye uzito wa gram 862, vilivyofichwa pia katika vyombo vya kutunzia Mafuta ya nywele, vilikamatwa katika kampuni hiyo hiyo mnamo Septemba 6, huku vilikuwa vinaelekezwa nchini Uingereza.
Aidha, vidonge 525 vya Tramadol 225mg na Ecstasy (MDMA) vilivyofichwa kwenye Pedi za kike vilikamatwa katika kampuni nyingine ya usafirishaji jijini Lagos mnamo Septemba 3, wakati mshipa wa Madawa ya kulevya 200 wa Promethazine na Pentazocine vilivyofichwa kwenye Chakula na Mimea vikiwa vinaelekea London vilikamatwa mnamo Septemba 4.
Babafemi alibainisha kuwa, walikamata tena Tramadol 225mg iliyofichwa kwenye mbegu za Mimea kutoka Cameroon kuelekea Afrika Kusini mnamo Septemba 6.
Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Port Harcourt, vidonge 550,000 vya Tramadol vilikamatwa mnamo Septemba 2 wakati wa uchunguzi wa pamoja na Wahudumu wa Huduma ya Forodha ya Nigeria
Katika Jimbo la Ekiti, NDLEA kwa ushirikiano na Jeshi la Nigeria walivamia kambi tatu ndani ya hifadhi ya Msitu wa Ise-Ekiti mnamo Septemba 3, ambapo zaidi ya kilo 100,000 za Bangi zilizokuwa kwenye ekari 51 za Ardhi ziliharibiwa, Watu wanane walikamatwa wakiwa na Madawa ya kulevya mbalimbali mnamo Septemba 6 katika Jimbo la Kaduna.
Matukio haya yanaonyesha jitihada za shirika hilo kupambana na biashara haramu ya Madawa ya kulevya na kuimarisha usalama wa taifa.