Makamu wa Rais wa Jamhuru ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdory Mpango amesema sababu mojawapo ya uharibifu wa mazingira ni sheria kinzani iliyounda wakala wa hifadhi za misitu TFS inayoufanya mkaa kuwa chanzo cha mapato ya wakala hiyo kutokana na vibali vinavyotolewa kwaajili ya kukata miti ya kutengeneza mkaa.
Dkt. Mpango ameelekeza hayo jijini Dodoma katika mkutano maalum wa wadau wa mazingira kuhusu mwelekeo wa mazingira nchini unafanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete.
“Nchi yetu inalia hali ya mazingira sio nzuri na hii inatokana na sababu mbalimbali mojawapo ni sheria kinzani kama sheria inayounda TFS bado inafanya mkaa kuwa chanzo cha mapato na hii inahamasisha utoaji wa vibali vya kukata miti kwaajili ya kutengenezea mkaa vilevile kasi ya upandaji miti ni ndogo kuliko kasi ya ukataji miti, pamoja na jitihada tunazoziona za Elimu mashuleni,jitihada za wasanii bado Elimu kwa umma haitoshi” Dkt. Philip Isdory Mpango
Mbali na hilo Dkt. Mpango amehiza elimu itolewe kuhusu biashara ya Hewa Ukaa (Carbon) ambayo ni chanzo kikubwa cha mapato ameelekeza fedha zinazopatikana kupitia biashara hiyo inayoendelea katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo wilaya ya Tanganyika mkoa wa Katavi itumike katika kuhifadhi mazingira na kukabiriana na mabadiliko ya Tabia nchi.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Ashatu Kijaji amesema silerikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais inaendelea kutoa elimu ya biashara ya hewa ukaa ‘Cabon’ ambayo ambayo ni biashara mpya inayosaidia uhifadhi wa mazingira pia ameiihiza jamii kutumia nishati Safi ya kupikia ili kuunga mkono jitihada za Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akizungumza kwa niaba ya Chama cha Mapinduzi,Katibu mwenezi wa CCM mkoa wa Dodoma Jawadu Mohamed amesema kukosekana usimamizi na ulinzi wa mazingira unachangia uharibifu miundombinu inayojengwa na serikali.