Kisa kingine cha moto shuleni kiliripotiwa katika Shule ya sekondary ya Wavulana ya Isiolo Boys siku ya Jumanne jioni.
Katika taarifa, Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya lilisema timu ya kukabiliana na tukio hilo ilikuwa imetumwa.
Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.
Haya yanajiri wakati kuna milipuko ya matukio ya moto shuleni kote nchini.
Kisa cha moto katika Shule ya Upili ya Wavulana ya Isiolo kinakuja siku tatu tu baada ya moto mwingine kuripotiwa katika Shule ya Upili ya Wasichana ya Isiolo.
Kisa hicho pia kinajiri siku chache baada ya moto katika shule ya Hillside Endarasha huko Nyeri kuwaua wanafunzi 21.
Wachunguzi bado wanafuatilia kisa hicho ili kujua chanzo cha moto huo.
Siku ya Jumatatu, Rais William Ruto alifanya mkutano na viongozi kutoka wizara ya Mambo ya Ndani na Elimu.
Ruto aliagiza kukamilika kwa haraka kwa uchunguzi kuhusu mkasa wa moto wa shule ya Hillside Endarasha Academy