Kamala Harris na Donald Trump wamepambana usiku wa kuamkia leo wakati wa mdahalo wa televisheni ulioandaliwa na ABC.
Wagombea hao wawili wa uchaguzi wa urais wa Novemba 5 wamekabiliana na maono yao yanayopingana kuhusu Marekani, chini ya miezi miwili kabla ya uchaguzi.
Mdahalo huo wa kwanza baina yao umefanyika huko Philadelphia usiku wa kuamkia hii leo.
Makamu wa rais wa chama cha Democratic na mgombea wa chama cha Republican, ambao hawakuwahi kukutana ana kwa ana, wamejikita kuhusu masuala muhimu ya uchaguzi wa Novemba ikiwemo uchumi, usalama wa mipaka na uhamiaji, sheria za utoaji mimba, mzozo wa mashariki ya kati, vita vya Ukraine pamoja na masuala mengine ya kimataifa.
Trump amesema kiwango cha mfumuko wa bei kwa sasa nchini Marekani kinatisha na kujitapa kwamba alipokuwa madarakani kati ya mwaka 2017 hadi 2021 aliimarisha uchumi wa taifa hilo
Kwa upande wa Harris pia