Msafara wa Umoja wa Mataifa uliokuwa umebeba wafanyakazi kwa ajili ya kampeni ya chanjo ya polio huko Gaza ulishikiliwa na watu wenye mtutu wa bunduki katika kituo cha ukaguzi cha jeshi la Israel, msemaji wa Umoja wa Mataifa alisema, akiongeza kuwa risasi zilifyatuliwa na magari yake kupigwa na tingatinga.
Stephane Dujarric, msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, alitaja tukio hilo lililotokea Jumatatu, “mfano wa hivi karibuni zaidi wa hatari zisizokubalika na kizuizi ambacho wafanyikazi wa kibinadamu huko Gaza wanapitia” na vikosi vya Israeli.
Alisema msafara huo ulikuwa umebeba wafanyakazi 12 wakielekea kuunga mkono kampeni ya polio katika eneo la kaskazini mwa Gaza.
“Harakati za kundi hilo ziliratibiwa kikamilifu na vikosi vya Israeli, na maelezo yote yalitolewa kabla ya wakati,” Dujarric alisema.