Cristiano Ronaldo ametoa maoni yake kuhusu hali ya Manchester United, akisisitiza kwamba timu hiyo kubwa haiwezi kusema kuwa haiwezi kushindana katika kushinda Ligi Kuu ya Uingereza au Ligi ya Mabingwa kila mwaka.
Akizungumza kwenye podcast ya Five, Ronaldo alisema, “Hii ni Manchester United! Unapaswa kuwa na mtazamo wa kisaikolojia wa kusema… labda hatuna uwezo huo, lakini siwezi kusema hivyo, Tunahitaji kujaribu, Unapaswa kujaribu.”
Ronaldo aliongeza kuwa ni muhimu kwa Manchester United kuijenga upya timu yao, pia alitoa ushauri kwa kocha Erik ten Hag, akisema kuwa kama angetafuta msaada kutoka kwa Wachezaji wa zamani kama Ruud van Nistelrooy, huenda angefaidika kwani wanajua klabu hiyo vizuri.
Aliendelea kuwataja Wachezaji wengine wakongwe kama Rio Ferdinand, Roy Keane, Paul Scholes, Gary Neville na Kocha mkongwe Sir Alex Ferguson, akisisitiza kuwa klabu inahitaji kusikiliza ushauri wao.
“Huwezi kujenga klabu bila maarifa,” Ronaldo alihitimisha.