Lael Wilcox, mwanariadha wa baiskeli wa “ultra-endurance” kutoka Alaska, ameweka rekodi mpya ya kuwa mwanamke mwenye kasi zaidi kuzunguka dunia kwa baiskeli.
Wilcox alikamilisha safari ya kilomita 29,169 (maili 18,125) kwa muda wa siku 108, saa 12 na dakika 12, akianza na kumaliza jijini Chicago.
Aliipiku rekodi ya awali iliyowekwa na Jenny Graham wa Scotland mwaka 2018, ambaye safari yake ilichukua siku 124, Wilcox alipitia nchi 21 kwenye Mabara manne, akiendesha hadi masaa 14 kwa siku na Safari hiyo sasa inasubiri kuthibitishwa na Guinness World Records.
Wilcox anajulikana pia kwa kushinda mbio ndefu za TransAm na kuweka rekodi katika Tour Divide, mbio zinazopitia Milima ya Rocky Marekani.
Aidha, Rekodi yake ya sasa inatarajiwa kuvutia wanariadha wengine wa kike duniani kote.