Justin Timberlake amefikia makubaliano ya kutatua kesi yake ya kuendesha gari akiwa amelewa huko Hamptons, vyanzo vinavyofahamu suala hilo viliiambia ABC News.
Mwanamuziki huyo wa muziki wa pop anatarajiwa kufika katika mahakama ya Sag Harbour Village siku ya Ijumaa kukiri hatia na kulipa faini, kusuluhisha mashtaka ya makosa hayo, vyanzo vilisema.
Wakili wake hakuwa na maoni yoyote .
Timberlake alikuwa akiondoka katika Hoteli ya Marekani mwezi Juni akiwa kasi ndipo aliposimamishwa kisha Afisa huyo alinusa pombe kwenye pumzi yake, kulingana na ripoti ya polisi.
Katika malalamiko ya jinai, polisi waliongeza kuwa Timberlake alikuwa na macho mekundu yaliyolegea sana na alikuwa anaongea polepole, hakuwa thabiti kwenye miguu yake na alifanya vibaya kwenye mtihani wa utimamu , kulingana na malalamiko.
Malalamiko ya jinai yalibainisha kuwa Timberlake alimwambia afisa aliyemkamata kua alikuwa amekunywa kinywaji kimoja tu.