Imeelezwa kuwa, uwepo wa reli ya kisasa na ya kwanza Afrika Mashariki na kati inayoendeshwa kwa nishati ya umeme (SGR) na yenye mwendo kasi usiopungua kilometa 160 kwa saa ni kiashiria kuwa nchi ina umeme wa kutosha.
Hayo yameelezwa leo tarehe 12 Septemba, 2024 na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko mara baada ya kuwasili jijini Dodoma akitokea jijini Dar es Salaam kwa SGR.