Wafanyakazi wa viwanja vya ndege nchini Kenya wameamua kusitisha mgomo na kurudi kazini baada ya kufikia makubaliano na serikali.
Katika makubaliano hayo ya kurudi kazini kwa wafanyakazi hao, serikali itaruhusu uchunguzi wa stakhabadhi kuhusu ukodishaji wa miaka 30 wa uwanja wa ndege wa JKIA na kampuni ya India ya Adani.
Gazeti la Nation Daily nchini Kenya, limebaini kwamba vyama vya wafanyakazi kwenye viwanja vya ndege vya JKIA pamoja na vile vya Mombasa na serikali kufuatia mkutano kati ya Waziri wa Uchukuzi Davis Chirchir, Viongozi wa Muungano wa wafanyakazi na katibu wa Muungano wa wafanyakazi nchini Kenya Cotu Francis Atwoli.
Waziri wa Uchukuzi Chirchir ameahidi kwamba mkataba ulioafikiwa kati ya serikali na kampuni ya Adani utawasilishwa mahakamani ambapo serikali imeshtakiwa ili kuruhusu uchunguzi wa wazi.
Katibu mkuu wa COTU Francis Atwoli amesema kwamba serikali imekubali kuanzisha mazungumzo ya mishahara na wafanyakazi mbali na makubaliano mapya ya majadiliano katika kipindi cha miezi miwili.