Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ‘HESLB’ inapenda kuwafahamisha Waombaji wa mikopo na Umma kwa ujumla zimebaki siku mbili za kufungwa kwa dirisha la maombi ya mikopo Elimu ya Juu 2024/25.
Kwa Mujibu wa bodi hiyo wakizungumza na millardayo.com ‘Tunapenda kuwataarifu waombaji wote wa Mikopo ya Elimu ya Juu tunatarajia kufunga dirisha la maombi ya Mikopo ifikapo tarehe 14, 09.2024 saa 5:59 Usiku .
Kila Mwombaji mwenye sifa anapaswa kuomba kabla ya tare na muda tajwa tapo juu.Hatua hii imechukuliwa ili kuwapa fursa wale ambao kwa sababu mbalimbali hawakuweza kufanya maombi ya mikopo katika muda uliokuwa umepangwa’- Mkurugenzi Mtendaji Dkt Bill Kiwia
Bodi inapenda kusisitiza kuwa hakutakuwa na muda mwingine wa nyongeza baada ya tarehe 14 Septemba, 2024.