Rais wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye, hapo jana alitangaza kulivunja bunge la kitaifa kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo, akitangaza kuwa uchaguzi mpya wa wabunge sasa utafanyika November 17.
Uamuzi wake umetokana na kile wengi wamesema ni kiongozi huyo kukosa uwingi wa wabunge kumuwezesha kupitisha bajeti na mabadiliko aliyoahidi wakati wa kampeni.
Faye alishinda urais mwezi Machi mwaka huu na kumteua Ousmane Sonko kama waziri mkuu, hata hivyo wamepata upinzani kutokana bunge la sasa kuwa na wabunge wengi wa rais aliyeondoka madarakani, Macky Sall.
“Serikali inasisitiza kuwa itaandaa uchaguzi bora na uhuru wa watu kujieleza na pia uhuru wa watu kuchagua, aliye bora ashinde.’’ Alisema rais Faye