Morocco imethibitisha kisa cha mpox kwa mtu mmoja katika jiji la Marrakech, wizara ya afya ilisema.
Haya ni maambukizi ya kwanza tangu mlipuko wa sasa kutangazwa kuwa dharura ya afya ya umma yenye kutia wasiwasi kimataifa na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) mwezi uliopita.
Tangazo hilo lilitolewa katika kukabiliana na kuenea kwa haraka kwa virusi vipya – clade, Afrika ya kati.
Mamlaka ya Morocco haijasema ni virusi gani mwanamume huyo anavyo.
Wizara ya afya ilisema anapokea matibabu na yuko katika hali nzuri.
Mamlaka ya Morocco inafuatilia afya ya watu wote ambao mtu huyo amewasiliana nao.
Hakuna aliyekuwa akionyesha dalili zozote, taarifa iliyotolewa Alhamisi alasiri ilisema.
Mpox inaweza kuenezwa kwa kukutana karibu na mtu aliyeambukizwa.